Mvua kubwa yanyesha Dar es Salaam alfajiri.

Mvua kubwa iliyoanza kunyesha Majira ya alfajiri leo katika jiji la Dsm imeendelea kuwatikisa wakazi wa jiji la Dsm hususan wakazi wanaishi pembezoni mwa Mito ambapo wakazi hao walilazimika kuzikimbia nyumba zao kunusuru maisha yao.

Katika eneo la Kigogo Manispaa ya Kinondoni jijini Dsm wakazi walionekana wamesimama pembeni mwa barabara kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji yaliyokuwa na kasi ambayo awali kabla ya kupungua barabara ya Kigogo Mburahati ilikuwa haipitiki kufuatia Maji kupita juu ya daraja.

Eneo la Kigogo Polisi Post Wakazi wa Mtaa huo nao walijikuta wakizikimbia nyumba zao kutoka na kasi ya Maji iliyoangusha baadhi ya nyumba ambapo baadhi ya wananchi wamedai chanzo cha mafuriko hayo ni daraja wanalodai limejengwa ndivyo sivyo.

Huko Kigogo Kisiwani na Mburahati nako hali haikuwa shwari kutokana na nyumba nyingi kuzingirwa na Maji ambayo yalianzia bonde la Sukita na kutawanyikia katika Makazi ya wananchi baada ya daraja la Kigogo kuzidiwa.

Hali kadhalika barabara kuu zikiwemo za Jangwani klabu ya Yanga, Kigogo na Mkwajuni pia hazikupitika kutokana Mafuriko.

Kutokana na hali ya mvua, Usafiri katika jiji la Dsm ulivurugika na kusababisha msongamano mkubwa wa magari kuelekea na kutoka katikati ya Mji na hivyo magari hayo kuchukua muda mrefu kufika yaendako.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Spika Ndugai aongoza mazishi ya Mbunge wa Newala.

Read Next

Waziri mkuu awasili Zanzibar ziara ya kikazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!