Spika Ndugai aongoza mazishi ya Mbunge wa Newala.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewaongoza Wabunge, Viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa na wakazi wa mkoa wa Mtwara kumzika aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Newala vijijini Ajali Rashid Akbar aliyefariki dunia akiwa hotelini kwake Mingoyo mkoani Lindi.

Marehemu Ajali Rashid Akbari alizaliwa January 25,1961 na kukutwa na umauti mnamo January 15 mwaka huu ambapo taarifa ya kifo chake iliyoelezwa na katibu wa bunge Steven Kagaigai imeeleza kuwa mbunge huyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kifo chake.

Spika wa bunge Job Ndugai amemuelezea mbunge huyo kuwa alikuwa mbunge mwenye kupigania maslahi ya wananchi wake hasa kwenye sekta ya maji na nishati.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na wenye ulemavu Jenister Mhagama akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali amesema kuwa mbunge huyo wakati wa uhai wake aliungana na serikali katika jitihada za kuwaletea maendeleo wakazi wa jimbo la Newala vijijini.

Marehemu akbar ameacha mjane na watoto wanne.

BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

China na Marekani zatia saini hatua ya kwanza ya mkataba wa kumaliza vita vya kibiashara.

Read Next

Mvua kubwa yanyesha Dar es Salaam alfajiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!