Wanaume zaidi ya 600 waripotiwa kupigwa na wenza wao.

Jumla ya wanaume 699 wameripotiwa kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kujeruhiwa kimwili mkoani Iringa katika kipindi cha mwaka 2018/19 sawa na asilimia 25.4 huku mengi ya matukio kama hayo yakifanyika bila ya kuripotiwa kutokana na mila na desturi za baadhi ya makabila mkoani humo.

Akisoma taarifa ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kikao cha kupitia mpango wa mawasiliano kuzuai ukatili kwa wanawake na watoto mkoani Iringa, Afisa Ustawi wa Jamii mkoani humo, Martin Chuwa amesema matukio mengi ya ukatili wa kijinsia kwa wanaume ambayo wanafanyiwa na wenza wao ni mengi lakini hayaripotiwi kutokana na mila na desturi za watu wa maeneo husika.

Serikali mkoani humo inakuja na moja ya mikakati kupambana na matendo ya ukatili wa kijinsia kwa ujumla wake kama inavyobainishwa na Mkuu wa Mkoa huo Ally Hapi.

Kwa upande wake mzee wa kimila kutoka kabila la Wahehe, Gerald Malangalila akawa na maoni juu ya kwanini wanaume wengi mkoani Iringa wanapigwa na wenza wao nab ado hawasemi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Bunge la Marekani na azimio kumng’oa Trump.

Read Next

China na Marekani zatia saini hatua ya kwanza ya mkataba wa kumaliza vita vya kibiashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!