China yasema ushindi wake katika mapambano na virusi vya korona ndio ushindi wa dunia.

An employee sprays disinfectant on a train as a precaution against a new coronavirus at Suseo Station in Seoul, South Korea, Friday, Jan. 24, 2020. China broadened its unprecedented, open-ended lockdowns to encompass around 25 million people Friday to try to contain a deadly new virus that has sickened hundreds, though the measures’ potential for success is uncertain. (AP Photo/Ahn Young-joon)

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi Hua Chunying amesema, hadi kufikia jana mchana, China imepokea msaada wa vitu vya kupambana na maambukizi ya virusi vya korona kutoka kwa serikali za nchi 21 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na China inapongeza na kushukuru jamii ya kimataifa kwa uelewa, uungaji mkono na msaada wake. Hua amesisitiza kuwa ushindi wa China ndio ni ushindi wa dunia, na China ina uwezo na imani ya kushinda vita hivyo.

Kwa mujibu wa Bi Hua Chunying, hadi kufikia jana mchana, nchi 21 ikiwemo Korea Kusini, Japan, Thailand, Malaysia, Indonesia, Kazakhstan, Pakistan, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Umoja wa Falme za Kiarabu, Algeria, Misri, na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF zimetoa msaada wa vifaa vya kuzuia na kudhibiti virusi vya korona kwa China, na pia serikali za nchi kadhaa zimeeleza matarajio ya kutoa msaada kwa China. Aidha, watu binafsi kutoka nchi mbalimbali pia wametoa msaada husika kwa China kwa njia mbalimbali. Bi. Hua anasema,

“Vitu vina gharama, lakini moyo hauna gharama. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki, tunawashukuru sana. China itaendelea kuwa na msimamo wa uwazi na kuwajibika kwa kiwango cha juu, na kupashana habari na kushirikiana na nchi mbalimbali duniani. China sio tu inalinda usalama wa maisha na afya ya watu wake, bali pia inafanya juhudi na kuchangia ulinzi wa usalama wa afya ya umma wa kikanda na kimataifa.”

Hivi karibuni, waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif baada ya kuongea kwa njia ya simu na mwenzake wa China Bw. Wang Yi, aliandika kwa lugha ya Kichina katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, akipongeza na kushukuru juhudi za China za kupambana na virusi hivyo na kusema “Iran na China ziko pamoja.”

Akizungumzia hilo, Bi. Hua amesema waziri Zarif ni waziri wa mambo ya nje wa kwanza duniani aliyetangaza hadharani kuunga mkono China, jambo ambalo limeonesha moyo wa dhati wa watu wa Iran kwa watu wa China, na pia uhusiano wa wenzi wa kirafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili. China inatoa shukrani kwa dhati uungaji mkono huo muhimu uliotolewa na marafiki wa Iran katika kipindi muhimu cha vita dhidi ya virusi.

Habari zinasema, rais Moon Jae-in wa Korea Kusini, waziri mkuu wa Cambodia Bw. Hun Sen pamoja na viongozi na watu wa hali mbalimbali wa nchi nyingine wamesema taabu ya China ni taabu yao. Bi. Hua anasema, “Ningependa kusema kuwa ushindi wa China ndio ushindi wenu, ushindi wa China ndio ushindi wa dunia. China inachukua hatua kali na za pande zote katika kupambana na maambukizi hayo. Jana tarehe 4, idadi ya wagonjwa waliopona na kutoka hospitali ilikuwa mara nne kuliko idadi ya wagonjwa waliokufa, na hadi jana, idadi ya wagonjwa waliopona imekuwa mara karibu mbili ya idadi ya vifo. China ina uwezo na imani ya kushinda maambukizi hayo mapema iwezekanavyo.”

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

CCM yasisitiza rushwa ni usaliti ndani ya chama.

Read Next

Nyumba zazingirwa na maji Tabora mjini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!