WHO yasema hakuna dawa za kutibu Virusi vya Corona.

Shirika la Afya duniani – WHO limepuua ripoti za vyombo vya habari za kuwepo kwa mafanikio ya dawa zinazovumbuliwa kuwatibu watu walioambukizwa virusi vipya vya corona, ambavyo vimesababisha janga nchini China na vimesambaa katika nchi nyingine karibu 20.

Ripoti ya televisheni moja ya China imesema watafiti katika Chuo Kikuu cha Zhejiang wamepata dawa inayofaa kutibu virusi hivyo, huku shirika la Sky News nchini Uingereza likiripoti kupigwa hatua muhimu katika kutengeneza chanjo.

Msemaji wa WHO Tarik Jasarevic amesema hakuna tiba zozote zilizothibitishwa mpaka sasa za virusi vya corona na kuwa WHO inapendekeza watu kujisajili katika mpango wa kufanya majaribio ya ufanisi na usalama wa dawa.

Mchakato wa kutengeneza na kuzifanyia majaribio dawa au chanjo dhidi ya aina mpya ya virusi kawaida huchukua miaka mingi na aghalabu hukumbwa na changamoto na mapungufu.

Idadi ya vifo vitokanavyo na virusi vya corona imekaribia watu 500 nchini China.

Comments

comments

clement

Read Previous

Maadhimisho ya Siku ya Sheria.

Read Next

Yanga yaufanya msimamo wa Ligi kuwa Mgumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!