Yanga yaufanya msimamo wa Ligi kuwa Mgumu.

Klabu ya soka ya YANGA imefanikiwa kufikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 17, na kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu, baada ya ushindi wa magoli 2-1 ilipocheza dhidi ya Lipuli FC ya Iringa.

Katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, goli la kwanza la Yanga lilipatikana kupitia mchezaji kiungo Mapinduzi Balama katika dakika ya 14 kwa kichwa cha mkizi akimalizia krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul.

Naye Kiungo Mghana, Bernard Morrison akakuza uongozi wa Yanga kwa kufunga bao la pili dakika ya 33 kwa shuti la mguu wa kulia akimalizia krosi ya iliyotokana kwa Juma Abdul pia.

Kwa upande wao Lipuli FC, walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 58 baada ya shuti la mpira wa adhabu liliupita ukuta wa Yanga na kipa wao Mnata.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga inazidiwa pointi nne na Azam FC na pointi 16 na vinara na mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo kwa pamoja wamecheza mechi mbili mbili zaidi.

Comments

comments

clement

Read Previous

WHO yasema hakuna dawa za kutibu Virusi vya Corona.

Read Next

Serikali haiendeshwi Kibabe – Majaliwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!