China yaelezea matumaini yake kukabiliana na Virusi vya Korona.

China imeelezea matumaini ya kuushinda ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona ambao mpaka sasa umesababisha vifo vya zaidi ya watu mia nane, huku wengine kadhaa wakiripotiwa kuambukizwa virusi hivyo kila siku.

Katika mazungumzo kwa njia ya simu, Rais wa China Xi Jinping amemuhakikishia Rais wa Marekani Donald Trump kwamba China itatokomeza ugonjwa huo hatari na kubainisha kuwa China ina imani na uwezo wake wa kupambana na janga hilo.

Kwa upande wake Rais Trump ameipongeza China kwa juhudi zake katika kukabiliana na virus vya Corona. Habari zinasema, viongozi hao wawili wamethibitisha pia ahadi yao ya kutekeleza hatua zilizoainishwa katika makubaliano ya kibiashara ya “hatua ya kwanza” yaliyotiwa saini mwezi uliopita na Marekani pamoja na China.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Zaidi ya 20 wauawa baada ya kushambuliwa na mwanajeshi Thailand.

Read Next

Ajali ya barabarani, wawili wafariki dunia 42 wanusurika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!