Zaidi ya 20 wauawa baada ya kushambuliwa na mwanajeshi Thailand.

Zaidi ya watu 20 wameuawa baada ya kushambuliwa na Mwanajeshi katika mji wa Nakhon Ratchasima nchini Thailand ambaye aliwafyatulia risasi kabla ya mshambuliaji huyo kuuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama,

Awali Mwanajeshi huyo Jakraphanth Thomma alimuua kamanda wa kambi ya jeshi na kupora bunduki ambayo aliitumia kufanya mauaji ya raia waliokuwa katika shughuli zao barabarani kwenye mji huo wa kibiashara ambao pia unafahamika kama Korat.

Habari zinasema Mshambuliaji huyo wanamume alikuwa akituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wakati anafanya mashambulizi kabla ya kuzingirwa usiku katika jengo alilokuwemo na hatimaye kupigwa risasi na kuuawa.

Waziri Mkuu wa Thailand Prayuth Chan-ocha ambaye ametembelea majeruhi katika hospitali waliyolazwa, amesema kwamba idadi ya waliopoteza maisha ni zaidi ya watu 20 ambapo watu wengine 57 wamejeruhiwa na kwamba inadaiwa kuwa shamabulizi hilo ni la kulipiza kisasi baada ya mshambuliaji huyo kuamini kwamba amelaghaiwa katika makubaliano ya kununua kipande cha ardhi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Bilioni tisa yafanikisha utekelezaji miradi kata ya Chanika.

Read Next

China yaelezea matumaini yake kukabiliana na Virusi vya Korona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!