Ramaphosa achukua mikoba ya Abdel Fattah Al Sis kama M/kiti wa AU.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekabidhiwa kijiti cha uongozi wa Umoja wa Afrika kwa kipindi cha mwaka mmoja kutoka kwa rais wa Misri Abdel Fattah al sisi, katika mkutano wa Umoja huo huko Addis Abeba nchini Ethiopia.

Akizungumza mbele ya viongozi wa Umoja wa Afrika, mawaziri, wanadiplomasia, rais wa Misri Abdel Fattah al sisi amesema ilikuwa ni fahari kubwa kwake kuwa kiongozi wa Umoja wa Afrika kwa kipindi cha mwaka mmoja. Amesisitiza kwamba yupo tayari kuandaa mkutano wa kilele wa kusaidia kuunda jeshi la Afrika kwa ajili ya kupambana na ugaidi.

Wakati wa hotuba yake, Cyril Ramaphosa amesisitiza juu ya utekelezaji wa Zlecaf, eneo la biashara huria la bara la Afrika, huku akitangaza kufanyika mkutano wa kilele wa Umoja huo Mei 2020 jijini Pretoria.

Cyril Ramaphosa amethibitisha pia kwamba ataitisha mkutano usiokuwa wa kawaida wa wakuu viongozi wa Umoja huo jijini Pretoria mwezi huo huo wa Mei kuzungumzia maswala ya usalama, mkutano ambao kauli mbiu yake itakuwa ni kukomesha mapigano.

Wazungumzaji wote katika kukao hicho wamegusia pia swala la Palestina na kubaini uungwaji wao mkono kwa madai ya Wapalestina. Katika hatua nyingine Cyril Ramaphosa pia alisema kwamba anaunga mkono haki ya kujitawala kwa watu wa Sahara Magharibi.

Comments

comments

clement

Read Previous

Watu 40,600 waambukizwa virusi vya Corona Duniani.

Read Next

Kinana na Yusuf Makamba waitikia wito wa kamati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!