Watu 40,600 waambukizwa virusi vya Corona Duniani.

Shirika la Afya Duniani limesema kuwa zaidi ya watu 40,600 wameambukizwa virusi vya Corona duniani. Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa leo vifo 908 vimetokea nchini China tangu Ugonjwa huo ulipoanza na watu 40,171 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini humo.

Kwenye mji wa Hong Kong pekee watu 36 wameambukizwa na mtu mmoja amekufa huku Macao ikiwa na wagonjwa 10 na wengi wa wagonjwa na vifo vimetokea kwenye jimbo la Hubei, ambako virusi hivyo vilizuka mwezi Desemba.

Licha ya kuonekana kwa jitihada kubwa za kudhibiti maambukizi haya nchini China, WHO inaonya kuwa iwapo maambukizi haya yataendelea kusambaa kwa watu ambao hawajaenda nchini China, basi itakuwa ni hatari zaidi.

Wakati huo huo, serikali ya Uingereza imeonya kuwa mlipuko wa virusi vya Corona ni kitisho kikubwa na imetangaza kuchukua hatua mpya za kuulinda umma. Wizara ya afya imesema leo kuwa maambukizi ya virusi hivyo ni kitisho kikubwa kwa afya ya umma nchini humo ambapo mpaka sasa jumla ya watu nane wameshaambukizwa Ugonjwa huo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Frederick Sumaye, arejea CCM.

Read Next

Ramaphosa achukua mikoba ya Abdel Fattah Al Sis kama M/kiti wa AU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!