Mkakati wa pamoja kukabiliana na majanga ya moto Nyanda za Juu Kusini.

Kufuatia hekta 600 za misitu kuteketea kwa moto katika shamba la Serikali la misitu la Sao Hill, wilayani Mufindi Mkoani Iringa kipindi cha mwezi Septemba na Oktoba, mwaka jana, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imesema imefika wakati kuundwa kwa mkakati wa pamoja kukabiliana na majanga ya moto Nyanda za Juu Kusini.

Uanzishwaji wa Ushirika kwa lengo la kukabiliana na majanga ya moto na uharibifu wa mazingira, umetajwa unaweza kuwa ni suluhisho la kuokoa misitu isiendelee kuteketea kwa moto na hivyo kusaidia taifa kukuza uchumi kupitia rasilimali za misitu nchi.

Wadau wa misitu kutoka mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma waliokutana Njombe kwa ajili ya kuweka mikakati jumuishi ya namna ya kupunguza matukio ya moto nyanda za juu kusini wamezungumzia njia bora za kukabiliana na matukio ya moto kwenye misitu.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri aliyekuwa mgeni rasmi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William wanasisitiza umuhimu wa kusimamia na kutunza rasilimali ya misitu.

Comments

comments

clement

Read Previous

Wilaya ya Mufindi yapewa siku 14 kumaliza Hospitali.

Read Next

TCRA yaadhimisha siku ya usalama mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!