Mkuu wa Mkoa akerwa watendaji kutolipa deni.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amewaagiza watendaji wa mitaa mitano inayounda Kata ya Mugusu katika Halmashauri ya Mji wa Geita kulipa mara moja deni la zaidi ya shilingi Milioni 1 kwa Maduhu Meli, Mkazi wa Mtaa wa Manga kwenye kata hiyo aliloikopesha Serikali ya Mtaa huo kwa ajili ya kununulia vifaa vilivyotumika kuchimba msingi na kujenga Kituo cha Afya, miaka miwili iliyopita.

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye amefika katika mtaa huo kwa ajili ya kuhamasisha shughuli za maendeleo akitumia ubao wa kufundishia,mithili ya mwalimu awapo darasani ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mwananchi huyo aliyeomba kusaidiwa kwa kile alichodai amekuwa akipigwa danadana kila uchwao.

Aidha akaonya tabia ya baadhi ya viongozi kuvamia na kujimilikisha maeneo ya Hifadhi kwa shughuli za kibinadamu.

Comments

comments

clement

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli azindua Wilaya Mpya ya Kigamboni.

Read Next

Waliofariki dunia China kutokana na Corona waongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!