Waliofariki dunia China kutokana na Corona waongezeka.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya Corona nchini China imeongezeka na kufikia 1016 ambapo Mamlaka ya Afya nchini humo imesema uwezekano wa vifo kuongezeka ni mkubwa kutokana na kuongezeka kwa maambukizi.

Mamlaka hiyo imesema kuwa mpaka sasa watu walioathirika na virusi hivyo ni 42,638 idadi ambayo ni kwa China pekee na kati yao wagonjwa 7333 wako mahututi huku watu wengine 21,657 wanahisiwa kuwa na virusi hivyo ambapo idadi ya walioruhusiwa kutoka Hospitalini baada ya kupatiwa matibabu imeongezeka na kufikia 3996.

Nchini Marekani watu 11 wamethibitika kuwa na virusi vya Corona ambapo tayari wamewekwa chini ya uangalizi maalum.

Aidha Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini katika msimu wa majira ya joto unaokuja utasaidia kumaliza mlipuko wa virusi hivyo ambavyo vinaendelea kuenea katika mataifa mbalimbali Duniani.

Mapema jana Rais wa China, Xi Jinping aliwatembelea wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona pamoja na maafisa wa afya ambao wanawahudumia wagonjwa hao, ambapo alisema virusi vya Corona kama janga na kwamba China itaendelea kuchukua hatua thabiti za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo ambapo pia amemteua Waziri Mkuu Li Keqiang kuongoza kundi la wafanyakazi litakaloshughulikia mlipuko wa virusi hivyo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Mkuu wa Mkoa akerwa watendaji kutolipa deni.

Read Next

Wilaya ya Mufindi yapewa siku 14 kumaliza Hospitali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!