Wilaya ya Mufindi yapewa siku 14 kumaliza Hospitali.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ametoa muda wa siku 14 kwa wakuu wa idara za manunuzi ya umma na fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kushughulikia changamoto za kimawasiliano miongoni mwao ili kukamilisha mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ambao umekwama katika hatua za mwisho.

Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo wakati akiwa katika ziara ya kushtukiza katika eneo la ujenzi wa hospitali hiyo wilayani Mufindi na kubaini hali ya mawasiliano mabovu baini ya idara ya manunuzi na idara ya fedha kiasi cha kusababisha ujenzi huo kwenda kwa kusuasua katika hatua za mwisho.

Amesema serikali mkoani humo haiwezi kukubali mradi wowote wa maendeleo kukwama kwa uzembe wa mtu au kikundi cha watu kwani miradi hiyo hugharimu mamilioni ya fedha za umma.

Comments

comments

clement

Read Previous

Waliofariki dunia China kutokana na Corona waongezeka.

Read Next

Mkakati wa pamoja kukabiliana na majanga ya moto Nyanda za Juu Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!