Idadi ya waliofariki kwa mafuriko Iringa yaongezeka.

Idadi ya watu waliofariki katika mafuriko yaliyotokea katika tarafa ya Idodi na Pawaga kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa imeripotiwa kuongezeka na kufikia watu watano huku wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo wakiendelea kuungana na serikali katika kukabiliana na madhara yaliyotokana na maafa hayo.

Akiongea wakati wa zoezi la kupokea msaada wa magodoro 100 kutoka na Shirika la World Vision yenye thamani ya shilingi milioni 15, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wapa Mkwewe amesema mtu mmoja kutoka tarafa ya Isimani ameripotiwa kufa kutokana na mafuriko hayo na kufanya jumla ya watu waliopoteza maisha katika maafa hayo kufikia watu watano.

Kwa upande wake Meneja wa World Vision Kanda ya Kati, Faraja Kulanga amesema wameamua kuunga mkono juhudi za serikali kupunguza makali ya athali zilizotokana na mafuriko hayo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema kwa sasa wanakabiliwa na upungufu wa dawa na vifaa vingine.

Comments

comments

clement

Read Previous

Uturuki yaapa kulipiza kisasi dhidi ya Syria.

Read Next

Maazimio ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!