Uturuki yaapa kulipiza kisasi dhidi ya Syria.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameionya serikali ya Syria kwamba italipa gharama kubwa kutokana na mashambulizi yake dhidi ya majeshi ya Uturuki katika eneo la kaskazini mashariki mwa Syria.

Wanajeshi watano wa Uturuki waliuawa katika mji wa Idlib unaodhibitiwa na upinzani siku ya Jumatatu wiki hii wakati majeshi ya Syria yakiendelea kusonga mbele katika eneo la mapigano.

Wanajeshi wa Uturuki walifyatua makombora kadhaa ili kujibu mashambulizi hayo, lakini Rais Erdogan amesema wataendelea na mashambulizi ya kujihami.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

TRA yamtoza mfanyabiashara wa pembejeo shilingi milioni 9.

Read Next

Idadi ya waliofariki kwa mafuriko Iringa yaongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!