Serikali yasaini makubaliano ya mkopo wa Tsh. Trilioni 3.3 .

Serikali imesaini makubaliano ya mkopo wa shilingi trilioni 3.3 kutoka kwa wakopeshaji 17 walioratibiwa na Benki ya Standard, ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuimarisha miradi ya maendeleo nchini.

Akizungumza katika hafla kusaini makubaliano hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema fedha hizo zinatarajia kuendeleza ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa awamu ya pili kutoka Morogoro hadi Makatupora akisema tukio hilo ni la kihistoria.

Dkt. Mpango amesema uendelezaji wa ujenzi wa mradi huo utasaidia kuongeza ajira kwa wazawa sambamba na kutumia vifaa kutoka Tanzania kama vile Saruji na vifaa vingine vya Ujenzi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank ya Standard Charter Sanjay Rughan amesema tukio la Serikali ya Tanzania kupatiwa mkopo ni sehemu ya kuunga mkono miradi ya kimkakati ikiwa ni uwekazaji mkubwa kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Hafla ya utiaji saini wa mradi huo wa makubaliano ya mkopo huo imehudhuriwa pia na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florence Luoga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa wakiwemo pia Mabalozi wa Denmark na Sweden nchini Tanzania.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

TMA yatoa utabiri wa hali ya hewa.

Read Next

Idadi ya vifo vya Corona yapanda kwa kasi China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!