Leo ni siku ya Radio Duniani.

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya Radio, vyombo vya habari vinatajwa kuwa na mchango mkubwa katika ushawishi wa mambo chanya katika jamii kwa kuwa vimebeba jukumu la kutoa taarifa zenye ujumbe sahihi unaoweza kusababisha nchi kupiga hatua kutoka sehemu moja kwenda nyingine kimaendeleo.

Katika taarifa yake ya maadhimisho ya siku ya Radio duniani leo, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema hadi februari 12, mwaka huu jumla ya redio 204 zimesajiliwa hapa nchini ambapo redio 183 ni zile zinazorusha matangazo katika masafa ya radio na 21 ni radio za mtandao hali inayowafanya watanzania kupata haki ya msingi ya kikatiba ya kupata taarifa.

Akizungumza na Channel Ten Mtangazaji Mkongwe aliyefanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini Eddah Sanga amesema siku hii inapaswa kutumiwa na wanahabari kuchambua masuala muhimu na yenye tija ili jamii ipate kujua nafasi ya Radio kwa maendeleo ya Taifa.

Pamoja na mambo mengine Eddah amesema licha ya kuwepo kwa mitandao mbalimbali ya kijamii ambavyo kila moja kwa nafasi yake ina uhuru wa kutoa taarifa lakini isiwe kigezo cha wanahabari kushindwa kufanya kazi zao kwa weledi na kwa misingi inayokubalika na taaluma hiyo.

Pia Channel Ten imefanya mahojiano na Watangazaji Wakongwe na Mashuhuri hapa nchini akiwemo Thecla Gumbo ambae alianza Utangazaji katika kituo cha Radio Tanganyika mwaka 1961 pamoja na Deborah Mwenda ambao wameelezea Uzoefu wao katika Tasnia ya Utangazaji na ushauri wao kwa Watangazaji wa kizazi cha sasa.

Maadhimisho ya siku hii ya Radio yamekwenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Kuhusisha kila mtu wa jinsia zote katika Radio”.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Papa Francis akataa pendekezo la Jimbo la Amazon – Marekani.

Read Next

Kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!