TMA yatoa utabiri wa hali ya hewa.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imetoa utabiri wa mvua za masika kwa kipindi cha Machi hadi Mei 2020 kuwa zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya mkoa wa Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba, maeneo mengi ya mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, mashariki mwa mkoa wa Geita pamoja na mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara.

Akitoa utabiri huo, mkurugenzi mkuu wa TMA, Dkt. Agness Kijazi amesema maeneo ya mkoa wa Kagera, magharibi mwa mkoa wa Geita, kaskazini mwa mkoa wa Kigoma, Dar es salaam, Pwani pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.

Na hapa Dkt. Kijazi anatahadharisha athari ambazo zinaweza kutokea kufuatia mvua hizo ambazo zitakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.

Kuhusu tishio la nzige ambao tayari wapo katika nchi jirani Dkt. Kijazi amesema kuhusu kuingia nchini ama la itategemeana na hali ya upepo kama anavyofafanua.

Kwa upande wa kuongezeka kwa viwango vya joto katika baadhi ya maeneo nchini inatarajiwa hali hiyo kuendelea hadi pale mvua zitakaponyesha.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Read Next

Serikali yasaini makubaliano ya mkopo wa Tsh. Trilioni 3.3 .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!