Kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali itaendelea kuhakikisha wanawake wanapata fursa za haki na usawa katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati madhubuti kuzuia na kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wizara ya Afya na Waasisi wa Umoja wa Jumuiya ya Wanawake katika Nchi Huru za Afrika (PAWO), uliolenga kuboresha Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000, Waziri Mwalimu amesema Serikali imeweka mazingira bora ya sera yanayozingatia usawa.

Awali Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Umoja wa Jumuiya za Wanawake katika Nchi Huru za Afrika Lea Lupembe amesifu juhudi zinazofanywa na Serikali kutokomeza Vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Leo ni siku ya Radio Duniani.

Read Next

TMA yatoa utabiri wa hali ya hewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!