Idadi ya vifo vya Corona yapanda kwa kasi China.

China imetangaza visa 15,000 vya maambukizi ya virusi vya ugonjwa unaofahamika kama Corona huku kukiwa na ongezeko jipya la idadi ya vifo 242 katika Mkoa wa Hubei likiwa ni ongezeko kubwa zaidi kutokea ndani ya muda wa masaa 24 tangu kuzuka kwa Ugonjwa huo Desemba mwaka jana hali inayoendelea kuzua wasiwasi mkubwa nchini humo na ulimwenguni.

Kutokana na kuongezeka kwa Vifo hivyo katika Mkoa huo wa Hubei ulioko katika mji mkuu wa Wuhan Tume ya Afya nchini China imewafuta kazi maafisa wakuu wa Mkoa wa Hubei kutokana na kuongezeka kwa idadi ya vifo na maambukizi.

Takwimu hizi zinazotia wasiwasi zinachochea uvumi kwamba ukali wa ugonjwa huo wa matatizo ya kupumua unaosababishwa na virusi vya Corona, ambao kwa sasa unajulikana kama Covid-19, umekithiri mara dufu.

Mapema wiki hii shirika la Afya Duniani, WHO, lilitangaza ugonjwa wa Corona kama ni janga la dharura nchini China , lakini likaamua kutotangaza hali hiyo ya kiafya kama ilivyofanywa na ugonjwa wa homa ya nguruwe na Ebola.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali yasaini makubaliano ya mkopo wa Tsh. Trilioni 3.3 .

Read Next

Mfahamu Mtakatifu Valentine, mhubiri wa kikristo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!