Wafugaji Itilima wafikisha kilio kwa Waziri Mpina.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amekumbana na malalamiko katika mkutano wake wa kwanza wa hadhara wakati wa ziara yake mkoani Simiyu ambapo wafugaji wamelalamikia kero ya mifugo yao kukamatwa na kuuzwa kwa wafugaji wengine, hata pale hukumu inapoagiza warudishiwe mifugo yao, hakuna hatua zinazochukuliwa.

Wakitoa kilio chao kwa waziri Mpina katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Laini A na B wilayani Itilima, wafugaji hao wametaja idadi ya ng’ombe waliouzwa kinyemela na waliorudishwa baada ya mahakama kutoa hukumu kuwa warejeshwe kwa wenyewe bila mafanikio, hivyo wanamuomba waziri awasaidie kutatua mgogoro huo ili waweze kupata mifugo yao.

Hali hiyo ikamlazimu waziri wa mifugo na uvuvi kumuagiza mkuu wa wilaya ya Itilima amuite ofisini kwake mkuu wa pori la akiba la Maswa akutane na mwanasheria wa wizara ya mifugo na mkurugenzi wa huduma za mifugo pamoja na wafugaji wanaolalamikia mifugo yao kuuzwa na kisha majibu ya kikao hicho ayapate mara moja.

Comments

comments

clement

Read Previous

Maziko ya Daniel Arap Moi, Maelfu ya raia wamiminika Kabarak.

Read Next

Mvua yapandisha bei ya Nyanya na Vitunguu Pwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!