Zoezi la uboreshaji daftari la kudumu Dsm.

Leo ni siku ambayo zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura jijini Dar es salaam na Pwani limeanza rasmi, zoezi litakalodumu kwa muda wa siku saba.

Channel ten ilitembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ambayo ni vituo vya kuboreshea daftari hilo na kujionea mwamko wa wananchi wa Dar es Salaam katika kuboresha taarifa zao kwenye daftari hilo la kudumu la wapiga kura.

Akizungumza ofisini kwake na kituo hiki, mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Aron Kagulumjuli amesema kinondoni inamajimbo mawili Kawe na Ubungo na jumla ya vituo vya kuboreshea daftari ni 372 ambapo jimbo la kawe linajumla ya vituo 190 na jimbo la kinondoni vituo 182.

Amesema zoezi hilo ambalo litakwisha tarehe ishirini ya mwezi huu linawahusu makundi matatu, likiwamo kundi la wale ambao hadi wakati wa kupiga kura watakuwa wametimiza miaka kumi na minane wale ambao wamehama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine pamoja na wale ambao kadi zao za kupiga kura zimepotea au kuharibika.

Je wananchi walifika kwenye vituo vya uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura nao wananini la kusema juu ya zoezi hilo na kwa watanzania kwa ujumla?

Ili mtanzania yoyote yule mwenye umri wa miaka kumi na minane aweze kupita kura kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu ni lazima awe ameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwenye eneo husika.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Bima yatakiwa kusaidia uchumi wa viwanda.

Read Next

Mwili wa Iddi Simba wazikwa makaburi ya Mwinyimkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!