Dkt. Shein akutana na Waziri Mussa Azzan Zungu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemuhakikishia kumpa ushirikiano mkubwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais, Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake hasa yale yanayohusu Muungano.

Dkt. Shein aliyasema hayo leo, Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais, Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ili kushika wadhifa huo.

Katika maelezo yake Rais Dkt. Shein alimueleza Waziri huyo kuwa yeye mwenyewe pamoja na viongozi wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo Mawaziri wake watahakikisha wanampa ushirikiano mkubwa Waziri huyo ili aweze kutekeleza vyema kazi zake.

Rais Dkt. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa miongoni mwa majukumu yake makubwa aliyonayo moja wapo ni kuhakikisha jitihada za waasisi wa Taifa hili Hayati Mzee Abeid Amani Karume na Hayati Julius Kambarage Nyerere za kuleta Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinaendelezwa na zinadumishwa.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais, Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu alitoa shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kupata uteuzi huo ambao aliahidi kuufanyia kazi kwa ufanisi pamoja na kuutendea haki.

Waziri Mussa Azzan Zungu ambaye alikuwa amefuatana na Mkurugenzi wa Muungano Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, alimueleza Rais Dkt. Shein kuwa atahakikisha umoja, mshikamano, upendo na undugu uliopo kati ya Serikali, wananchi na viongozi wa Zanzibar na Tanzania Bara unadumishwa na kuendelezwa kwa manufaa ya Taifa lao.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mwili wa Iddi Simba wazikwa makaburi ya Mwinyimkuu.

Read Next

CCM mkoa wa Pwani waipongeza serikali kwa maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!