Mwili wa Iddi Simba wazikwa makaburi ya Mwinyimkuu.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wamewaongoza waombolezaji katika Mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Iddi Mohamed Simba aliyefariki dunia jana na kuzikwa leo katika Makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni jijini Dsm.

Viongozi wengine wastaafu waliohudhuria Mazishi hayo ni Pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, viongozi kutoka Taasisi na Mashirika ya Serikali pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza katika mazishi hayo Sheikh wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mjumbe wa baraza la Ulamaa waislam Bakwata Sheikh Shaban Juma Abdallah amewataka Waislam kuishi katika miongozo aliyotoa M/mungu kupitia Mtume wake Muhammad, lakini pia kukumbuka kuwa Maisha ya Dunia ni Mafupi na yanahitaji Maandalizi mazuri kabla ya kurudi kwa Muumba.

Awali Waumini wa Kiislam katika Msikiti wa Manyesha walipata Fursa ya Kumuombea Dua Marehemu pamoja na Kumswalia ambapo pia Masheikh wakiongozwa na m/kiti wa Baraza Kuu la Waislamu – Bakwata Sheikh Khamis Mataka walipata fursa ya Kumuelezea Marehemu katika Harakakati zake katika Mambo ya Dini.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Zoezi la uboreshaji daftari la kudumu Dsm.

Read Next

Dkt. Shein akutana na Waziri Mussa Azzan Zungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!