Sekta ya bima yahamasishwa kusaidia uchumi wa Viwanda.

Serikali imeitaka sekta ya bima nchini, kuhakikisha inatoa mchango utakaosaidia wazalishaji wa malighafi kwenye viwanda vinavyoanzishwa nchini, hawatetereki katika uzalishaji, kutokana na majanga wanayoweza kuyapata.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shuguli za Bima (TIRA), na kusisitiza kuwa bila ya wazalishaji wa malighafi kulindwa na bima, lengo la kuwa na uchumi wa viwanda, halitaweza kufikiwa.

Mapema akimkaribisha Naibu Waziri Kufungua kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi (TIRA) na Afisa Mtendaji Mkuu Dkt. MUSSA JUMA, akaweka wazi mikakati waliyonayo, ya kuhakikisha wananchi wengi wanajiunga na bima mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupitia viwango vya tozo za bima na kuweka mifumo ya malipo ya kielektoniki, ili kudhibiti mapato yanayokusanywa.

Comments

comments

clement

Read Previous

Upanuzi wa Chanzo cha Maji, Kata ya Ikwiriri (W) Rufiji.

Read Next

Wachina wapambana na maambukizi ya COVID-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!