TANESCO yabaini wizi mkubwa wa umeme.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Dar es Salaam na Pwani limembaini mfanyabiashara wa Bar inayofahamika kwa jina la Backtown Jumanne maarufu kama J4 maeneo ya Manzese Bakheresa jijini Dar es salaam aliyejiunganishia umeme kwa njia za udanganyifu kwa miaka mingi akichezea mita.

Oparesheni hiyo ya kumbaini bwana Jumanne imefanywa na Mkuu wa Oparesheni Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mrisho Sangiwa ambaye amesema mfanyabiashara huyo amekuwa akiiba umeme tangu mwaka 2016, hali iliyosababisha kuikosesha hasara kwa Shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuikosesha Serikali kodi kutokana na kukwepa kulipa bili.

Baada ya maelezo hayo mwandishi wetu Said Makala alimtafuta kwa simu mfanyabiashara huyo na haya yalikuwa ni mazungumzo yake ambapo awali alionekana kumshawishi Mhandisi Mrisho kukutana nje ya utaratibu kwa ajili ya mazungumzo zaidi ili kuyamaliza.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wachina wapambana na maambukizi ya COVID-19.

Read Next

Bima yatakiwa kusaidia uchumi wa viwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!