Upanuzi wa Chanzo cha Maji, Kata ya Ikwiriri (W) Rufiji.

Serikali imekubali kutoa shilingi milioni mia moja tisini na tano ili kupanua chanzo cha maji kilichopo katika kata ya Ikwiriri wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Kauli hiyo aliitoa Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati alipofanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani na kutembelea chanzo cha maji cha Ikwiriri na baada ya kuridhishwa na mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo ndipo akakubali kutoa kiasi hicho cha fedha shilingi milioni mia moja tisini na tano huku akiridhishwa na utendaji wa kazi unaofanywa hapo, chini ya msimamizi wa mradi huo mhandisi JUMA DALLO.

Kabla ya kuridhishwa na mradi huo pia alimwagiza mkuu wa wilaya ya Rufiji kuhakikisha wanatatua changamoto ambazo zimebainika ili waweze kuwatatulia wananchi tatizo la maji na kaulimbiu ya kumtua mama ndoo kichwani iweze kukamilika.

Comments

comments

clement

Read Previous

Mfahamu Mtakatifu Valentine, mhubiri wa kikristo.

Read Next

Sekta ya bima yahamasishwa kusaidia uchumi wa Viwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!