CCM mkoa wa Pwani waipongeza serikali kwa maendeleo.

Serikali ya awamu ya tano imepongezwa kwa kuwapelekea wananchi maendeleo katika sekta mbalimbali za huduma na uchumi ikiwemo sekta ya mifugo ambayo kwa mara ya kwanza tangu uongozi wa serikali ya awamu ya tano, imefufua majosho ya kuogeshea mifugo pamoja na kuanza uzalishaji wa dawa za chanjo dhidi ya magonjwa yanayoshambulia mifugo hapa nchini.

Aidha serikali imefanikisha ujenzi wa kiwanda cha kuchakata nyama cha TANCHOICE kilichoko Kibaha mkoani Pwani, hivyo kuwahakikishia wafugaji wa mkoa huo na maeneo mengine ya Tanzania soko la uhakika la mifugo yao.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani katika mkutano uliofanyika kijiji cha Chamakweza Halmashauri ya Chalinze, wilayani Bagamoyo wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleleo inayotekelezwa kupitia ilani ya CCM ya mwaka 2015 /2020, amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi na uongozi thabiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Mbali ya miradi ya sekta ya mifugo, miradi mingine iliyokaguliwa na wajumbe hao ni pamoja na mradi wa nyumba za askari polisi uliogarimu zaidi ya shilingi milioni 700, Hospitali ya Kibaha mjini na Chuo cha uongozi cha CCM kilichoko Kibaha Kwa Mfipa.

CCM Mkoa wa Pwani kinaadhimisha miaka 43 ya Chama hicho leo mjini Kibaha.

Comments

comments

clement

Read Previous

Dkt. Shein akutana na Waziri Mussa Azzan Zungu.

Read Next

Kaya 227 waomba msaada wa chakula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!