Maambukizi ya virusi vya Corona yaongezeka Italia.

Serikali ya Italia imetangaza hali ya hatari katika maeneo yote ya nchi hiyo yenye watu wengi ikiwa ni katika harakati za kuendelea kupambana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona.

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuzuia raia wa nchi hiyo kutembea na kukutana katika maeneo ya umma, au kundi la watu wengi kuwa pamoja.

Waziri Mkuu Giuseppe Conte amewataka raia wa nchi hiyo kusalia nyumbani na kuomba kibali maalum iwapo wanataka kusafiri nje ya maeneo yao, hatua ambayo amesema inachukuliwa kwa sababu hakuna muda wa kupoteza kuhusu mapambano dhidi ya virusi hivyo.

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maambukizi hayo imeongezeka kutoka watu 366 hadi kufikia watu 463 na kulifanya taifa la pili lililoathiriwa zaidi na maambukizi haya duniani baada ya China ambapo maafisa wa Afya nchini humo wanasema kuwa majimbo 20 yameathiriwa na maambukizi hayo ya virusi vya corona.

Shirika la fya Duniani WHO linasema kuwa watu zaidi ya 3,800 wamepoteza maisha na wengine 110,000 kuambukizwa kote duniani, idadi kubwa wakiwa raia wa China.

Comments

comments

clement

Read Previous

Athari za mvua kubwa Morogoro.

Read Next

Kesi ya vigogo wa CHADEMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!