Virusi vya Corona vyazidi kuindama michezo.

Timu ya soka ya Juventus ya nchini Italia imethibitisha kuwa mchezaji wake Daniele Rugani amepata maambukizi ya virusi vya Corona licha ya tahadhari zinazoendelea kuchukuliwa na mamlaka za michezo na serikali kwa ujumla.

Kufuatia kisa hicho, Juve pamoja na chama cha soka cha Italia, wamesema kuwa watachukua hatua ikiwemo kuwachunguza na kuwalinda wachezaji wote ambao walishiriki pamoja na Rugani kwenye mechi ya ligi dhidi ya Inter Milan.

Wakati taarifa hizo zikitokea nchini Italia, mapema jana nchini Ujerumani kuna habari ziliwekwa bayana kuwa mchezaji wa klabu ya Hannover Ninety Six Timo Hubers amekutwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Zuio la safari za Ulaya kuingia Marekani.

Read Next

Rais Dkt. Magufuli amlipia Mbunge Peter Msigwa (CHADEMA).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!