Zuio la safari za Ulaya kuingia Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza kuweka zuio kwa raia wa nchi za Ulaya kuingia nchini Marekani ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Katika hotuba yake kwa njia ya Televisheni aliyoitoja jana siku ya Jumatano, amesema safari zote za kutoka Ulaya zitazuiwa kwa siku 30 zijazo lakini hatua kali zilizo na umuhimu hazitaihusisha uingereza ambayo mpaka sasa ina visa 460 vya virusi vya Corona vilivyothibitishwa.

Rais Trump amesema Mpaka sasa nchi ya Marekani ina visa 1135 vilivyothibitishwa nchini humo ambapo watu 38 kati ya hao wameripotiwa kupoteza maisha hivyo amesema hatua hiyo ya kuzuia safari za Ulaya itasaidia kuzuia visa vipya vya Maambukizi kuingia nchini humo na kuongeza kuwa zuio hilo litaanza kutekelezwa kuanzia usiku wa Ijumaa hapo kesho.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Changamoto ya maji taka mtaa wa Lindi Dsm.

Read Next

Virusi vya Corona vyazidi kuindama michezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!