WHO yatangaza Virusi vya Corona kuwa janga la dunia.

Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza virusi vya corona kuwa janga la kimataifa. Tangazo hilo limefuatia hatua za kupiga marufuku usafiri kati ya mataifa na kuahirisha matukio yanayowaleta pamoja watu wengi.

Miji kadhaa nchini Marekani imefuata mfano wa bara la Ulaya kufuta mikusanyiko yote mikubwa huku uamuzi wenye uzito zaidi ukiwa ni ule wa marufuku ya safari kati ya Marekani na Ulaya iliyotangazwa na Rais Donald Trump.

Tangazo hilo la WHO limesema kasi ya kuenea kwa virusi vya corona na ukali wake vimetokana na uzembe wa hali ya juu katika kuushughulikia ugonjwa huo.

Visa vya maambukizi ya virusi hivyo kote duniani vimeongezeka na kufikia watu 124,000, ambapo watu wapatao 4,500 wamekwisha kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa COVID 19, wengi wao nchini China, Italia na Iran.

Comments

comments

clement

Read Previous

Wananchi wajenga kituo cha afya, waiomba serikali vitendea kazi.

Read Next

Umoja wa Ulaya kutafakari marufuku ya usafiri ya rais Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!