Mwakinyo kwenda Ujerumani kesho kumkabili Culcay.

Bondia Hamis Mwakinyo anaondoka Nchini kwenda nchini Ujerumani ambapo tarehe 21 mwezi huu anatarajiwa kupanda ulingoni kumkabili bondia Jack Culcay kwa ajili ya kuwania mkanda wa WBO, pambano litakalochezwa nchini Ujerumani.

Mwakinyo ametamba kuwa amejiandaa vya kutosha kukabiliana na mpinzani wake na pia amemsoma kwaajili ya kukabiliana nae.

Adha Mwakinyo amebainisha kuwa mpambano huo kama akifanikiwa kushinda Utampa nafasi ya kumpandisha hadhi zaidi.

Mara ya mwisho Bondia Hassan Mwakinyo alipanda ulingoni November 30 Mwaka 2019 ambapo alishinda kwa pointi kutoka kwa Arnel Tinapay kutoka Philipino mpambano uliochezwa katika uwanja wa Taifa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali yahimiza matumizi sahihi ya maji.

Read Next

Wanafunzi 450 watoroka Bahi kwa kipindi cha miezi miwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!