Kambi ya Taifa Stars yavunjwa na Ligi zote zasimamishwa.

Muda mfupi baada ya serikali kusitisha shughuli zote za kimichezo zinazokusanya umati mkubwa wa watu ikiwa ni njia ya kudhibiti kuenea kwa maambukizi virusi vya corona, shirikisho la soka nchini TFF limetangaza kusimamisha ligi zote mchezo wa mpira wa miguu nchini kwa muda wa siku 30.

Shirikisho hilo pia limeivunja rasmi kambi ya timu ya taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars, ya kujiandaa na mechi za kufuzu mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Tunisia baadaye mwezi huu, na kambi ya kujiandaa na michuano ya CHAN.

Aidha, kutokana na agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, TFF imeitisha mkutano wa dharura wa Bodi inayosimamia ligi ili kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa agizo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Zaidi ya Walimu wakuu 270 wapatiwa mafunzo dhidi ya Corona.

Read Next

Watu wawili zaidi wagundulika kuwa na Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!