China maisha yameanza kurejea.

China leo imefikia hatua muhimu katika vita dhidi ya janga la virusi vya corona, baada ya kutangaza kutokuwepo na maambukizi mapya ya ndani kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mlipuko, lakini maambukizi ya kutoka nje yanahatarisha maendeleo hayo.

Mji wa Wuhan ambao ulikuwa kitovu cha mlipuko wa virusi vya corona mwezi Desemba, umeripoti kutokuwa na maambukizi mapya ya ndani, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mamlaka zilipoanza kuchapisha takwimu mnamo Januari mwaka huu.

Mji huo ulio na wakaazi karibu milioni 11 uliwekwa chini ya karantini kuanzia Januari 23, huku wakaazi wengine milioni 40 katika jimbo la Hubei nao wakifungiwa siku zilizofuata.

Maisha yameanza kurejea kama kawaida katika maeneo mengine ya nchi, huku watu wakirejea kazini, viwanda kufunguliwa na shule zikijiandaa kuendelea na masomo katika baadhi ya mikoa.

Comments

comments

clement

Read Previous

Spika wa Bunge asitisha ziara za kamati za kudumu za Bunge.

Read Next

Kukatika kwa mawasiliano ya barabara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!