DRC yatangaza wagonjwa 14 wa Corona.

In this Feb. 6, 2020, photo, a man tries on a face mask at a pharmacy in Kitwe, Zambia. The coronavirus that has spread through much of China has yet to be diagnosed in Africa, but global health authorities are increasingly worried about the threat as health workers on the ground warn they are not ready to handle an outbreak. (AP Photo/Emmanuel Mwiche)

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza wagonjwa 14 wa maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Homa kali ya mapafu Corona.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi ametangaza hatua za kukabiliana na kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo, ambao shirika la Afya Duniani, WHO, liliuita kuwa ni janga la kimataifa.

Daktari Jean-Jacques Muyembe, mratibu wa mapambano dhidi ya virusi vya Ebola, sasa ni mratibu wa mapambano dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Rais Felix Tshiskedi ameeleza kuwa janga hili ni kubwa na kwamba raia wanapaswa kuwa makini hususani kipindi hiki ambapo dunia inaangalia kupata tiba ya ugonjwa huo

Rais huyo pia amepiga marufuku Mikusanyiko yote, mikutano, sherehe za watu zaidi ya ishirini kwenye maeneo ya umma nchini kote huku shule na vyuo vikuu vikifungwa kwa mwezi mmoja kuanzia leo.

Aidha sherehe zote za ibada ya watu wengi na michezo katika viwanja mbalimbali na sehemu zingine za mikusanyiko pia zimepigwa marufuku.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Ukarabati wa Uwanja wa Taifa kubebwa na Serikali kwa asilimia kubwa.

Read Next

Magereza: Hakuna kutembelea wafungwa na mahabusu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!