Idadi ya Vifo Corona yafikia 4000 Italia.

Italia imesema idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya corona imepindukia 4,000, likiwa ni taifa liloathirika zaidi duniani.

March 20 mwaka huu inatajwa kuwa ni siku mbaya zaidi kwa Italia baada ya kuthibitisha vifo 600 ndani ya siku moja huku Asilimia 36.2 ya vifo vinavyotokana na virusi vya corona ulimwenguni kote vimerikodiwa Italia, taifa lenye watu milioni 60.

Aidha kiwango cha vifo nchini humo ni cha asilimia 8.6 kati ya wale walithibitishwa kuwa na maambukizo hayo, ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuliko taifa lingine lolote.

Duniani kote kumerekodiwa vifo 11,000 huku idadi ya maambukizi ya virusi hivyo ikifika 258,000.

Comments

comments

clement

Read Previous

JKT watekeleza mpango wa dharura wa kujitegemea kwa chakula.

Read Next

Uongozi wa U/Ndege Songea wachukua hatua za awali kudhibiti Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!