Star wa Muziki wa Country Duniani Kenny Rodgers afariki dunia.

Star wa Muziki wa Country Duniani Kenny Rodgers wa Marekani Amefariki Dunia akiwa na Umri wa Miaka 81, Wawakilishi wa Familia ya Kenny Rogers Wamethibisha kuwa Kenny Rodgers alipatwa na umauti akiwa Nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa wawakilishi hao Rodgers amefariki kwa amani akiwa chini ya Uangalizi wa Muuguzi huku akiwa amezungukwa na familia yake.

Kenny Rodgers Aliiteka dunia kuanzia miaka ya 70 na 80 ambapo pia alishinda tuzo 3 za Grammy, ambapo pia aliachia nyimbo maafuru ambazo ni The Gambler, Lucille Pamoja na Coward of the Country.

Kenny Rodgers ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo humo Georgia, Marekani alikuwa Mwandishi mahiri wa Nyimbo, Muigizaji, Muimbaji na ëmtayaraishaji wa kazi za muziki.

Katika kazi za uigizaji Rogers ametokea kwenye filamu mbalimbali ikiwemo Six Pack mwaka 1982, lakini pia akijizolea umaarufu kwenye tamthiliya kadhaa za runinga kama vile The Gambler franchise, Christmas in America na Coward of the County.

Comments

comments

clement

Read Previous

Mhisiwa wa Corona Lindi aruhusiwa.

Read Next

Waziri Mkuu aonya wanaopotosha kuhusu Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!