Takribani watu milioni 1.5 Uingereza watahadharishwa.

Serikali ya Uingereza imewataka takribani watu milioni 1.5 nchini humo ambao wapo hatarini zaidi na maambukizi ya Virusi vya Corona kujitenga kwa miezi mitatu ili kujiepusha na maambukizi hayo.

Miongoni mwao ni wenye saratani ya damu, magonjwa sugu ya mfumo wa upumuaji na waliofanyiwa upandikizwaji wa viungo. Taarifa ya serikali imesema, Shirika la Huduma za Afya la Uingereza NHS litawapelekea taarifa ya kimaandishi watu hao katika kipindi kifupi kijacho na kuwafahamisha hatua mahususi za kufuatwa.

Chama cha waandishi habari nchini Uingereza kimesema takribani watu 240 hadi sasa wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amenukuliwa akisema, serikali itachukua hatua ambazo hazijawahi kushuhudiwa, iwe katika amani au vita lakini ni za lazima zichukuliwe ili kunusuru taifa hilo na janga hilo

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Anusurika kifo kufuatia ajali ya barabarani Songea.

Read Next

Wafanyakazi watano wa TRC wafariki kwa ajali ya Treni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!