Vifo vya Corona Ujerumani vyaongezeka.

Idadi ya waliombukizwa virusi vya corona nchini Ujerumani imeongezeka na kufikia watu 22,672 huku waliokufa wakifikia 86.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa taasisi ya umma ya uratibu wa afya ya Robert Kock.

Kwa mujibu wa taasisi hiyo takwimu za jana Jumapili nchini humo zilionesha kuwepo kwa maambukizi 18, 610 na vifo 55, huku ikionya kwamba idadi inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo iliyoanishwa kwa kuwa si mamlaka zote za afya za majimbo zilizoweza kuwasilisha takwimu zao mwishoni mwa juma.

Wakati huo huo Kwa takribani mwezi mmoja Korea Kusini leo imeripoti kiwango cha chini cha ongezeko la visa vipya vya virusi vya corona.

Kwa mujibu wa kituo cha udhibiti magonjwa na kinga cha nchi hiyo (KCDC) kumerekodiwa maambukizi mapya 64, ikiwa ongezeko dogo tangu Februari 25, na kufanya idadi jumla ya maambukizi hayo kufikia watu 8,961.

Watu saba wengine ambao walifanyiwa vipimo vya ugonjwa wa COVID19 wamekufa na kufanya jumla ya vifo nchini humo kufikia 111.

Idadi kubwa ya waliokufa walikuwa wazee, ambao pia walikuwa na magonjwa mengine nyemelezi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Uboreshaji wa daftari la mpiga kura awamu ya kwanza.

Read Next

Wageni kutoka nje ya nchi wapungua kwa asilimia 99.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!