Wananchi walia na daraja kubomoka.

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini huku zikileta athari za uharibifu wa miundombinu wakazi wa mtaa wa Nguzo manispaa ya Morogoro wamelalamikia changamoto ya kubomoka kwa daraja linalounganisha njia ya kwenda hospitali ya rufaa ya Morogoro na makao makuu ya mkoa.

Wakizungumza katika tukio hilo na kushuhudia athari zilizojitokeza kufuatia kubomoka kwa daraja linalodaiwa kuathirika kufuatia kingo zake kujaa uchafu hali iliyopelekea maji kuharibu vibaya daraja hilo huku wakazi wa mtaa huo wakieleza namna wanavyopata changamoto za kubomoka kwa daraja hilo.

Aidha Mwenyekiti wa mtaa huo ameeleza hatua alizochukua mara baada ya kubainika kwa kuwepo kero hiyo huku meneja wa Tarura mkoa wa morogoro James Mnene akieleza mipango iliyopo katika kuhakikisha miundombinu yote iliyoharibika wakati huu wa mvua inafanyiwa marekebisho huku daraja hilo likiwa ni miongoni mwao.

Comments

comments

clement

Read Previous

Bilioni Moja kuongeza usikivu wa TBC Mikoa Mitano.

Read Next

Mahakama Kuu ya Tanzania na Mapambano dhidi ya Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!