Agizo la rais Magufuli latekelezwa kwa ubunifu Handeni.

Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli juu ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona limetekelezwa kwa namna ya kipekee wilayani Handeni mkoani Tanga baada ya madereva wa bajaji wilayani humo kufanya ubunifu wa kuweka mfumo maalum wa maji ya kunawa mikono kwenye usafiri huo ili kuwakinga abiria dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Ubunifu huo umeonekana wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe yenye lengo la kutembelea na kukagua utekezaji wa maagizo ya serikali juu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona ziara iliyofanyika kwenye maeneo ya vituo vya mabasi, masokoni, kwenye migahawa ya mama ntilie pamoja na kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga.

Baada ya hapo Mkuu huyo akaendelea na kutoa elimu ndani ya mabasi huku akisisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Wazee wa Kimila kufanya maombi dhidi ya Corona.

Read Next

Serikali yapokea msaada kukabiliana na Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!