Aliyevuka kwa kutoa Rushwa akamatwa.

Kikosi maalum cha kudhibiti Wimbi la wahamiaji haramu katika mipaka ya nchi idara ya Uhamiaji mkoa wa Mara kimefanikiwa kumkamata mama mmoja Raia wa Burundi Bi.Clarise Nimpaye aliyevuka mpaka kwa kutumia njia za rushwa ya shilingi 20,000 ili asikaguliwe na maafisa usalama kwa kuwa hakuna na vibali vya kumruhusu kuvuka mpaka wa Tanzania akitokea nchi ya Kenya.

Mama huyo amekamatwa katika kuzuizi cha Kirumi akiwa amesafiri umbali wa kilometa 60 kutoka eneo la Sirari Mpaka wa Tanzania na Nchi ya Kenya akihofia kumbukizwa vidusi vya Corona akiwa ugenini nchini Kenya.

Naibu kamishina wa Uhamiaji mkoa wa Mara Albert Rwelamira amewataka wananchi wanaoishi maeneo ya mipaka ya nchi kushirikiana na serikali kuwafichua wahamiaji haramu wanaovuka mipaka kwa njia ambazo hazijarasimishea kisheria ili kunusuru maambukizi mapya ya virusi vya Corona.

Comments

comments

clement

Read Previous

Idadi ya maambukizi ya Corona Afrika Kusini yafikia 709.

Read Next

Wazee wa Kimila kufanya maombi dhidi ya Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!