Idadi ya maambukizi ya Corona Afrika Kusini yafikia 709.

Afrika Kusini imesema idadi ya waliothibitika kuwa na virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 709 leo Jumatano kutoka 554 iliyoripotiwa jana ikiwa ni ongezeko la asilimia 28.

Afrika Kusini ambayo sasa ndio taifa lenye idadi kubwa ya maambukizi ya virusi hivyo katika bara la Afrika , tayari imetoa agizo la watu kujifungia ndani na kutotoka nje ovyo agizo ambalo litaanza kesho Alhamisi Machi 26.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Zweli Mkhize amesema ongezeko la idadi ya maambukizi ni kubwa ukilinganisha na idadi ya watu 554 jana huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka katika siku za usoni.

Kuanzia Jumatano wiki iliyopita Afrika Kusini ilifunga mipaka yake dhidi ya wageni wanaotoka katika nchi zenye mambukizi makubwa ya virusi vya Corona na shirika la ndege la taifa hilo lilisitisha huduma zake za usafiri za kimataifa, kikanda na kitaifa ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo.

Maambukizi ya kwanza nchini humo yaliripotiwa kuingizwa na raia kutoka bara la Ulaya lakini kwa sasa waziri huyo wa afya Mkhize amesema wamekuwa wakipata taarifa za maambukizi ya ndani.

Comments

comments

clement

Read Previous

Wahamiaji haramu 36 wakamatwa mkoani Mara.

Read Next

Aliyevuka kwa kutoa Rushwa akamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!