Mkuu wa Wilaya ya Kibaha asimamisha mnada mwezi mmoja.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Asumpter Mshama amewataka wafanyabiashara wa mnadani kufunga biashara zao kwa muda wa mwezi mmoja , baada ya maeneo wanayofanyia biashara ya mnadani kuwa katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 unaonezwa na kirusi cha Corona.

Pamoja na agizo hilo pia amewataka wamiliki wa bar na grocery kuhakikisha Wanafunga Saa Nne usiku na atakayekaidi atachukuliwa hatua.

Mkuu wa huyo wa Wilaya ya Kibaha Asumpaa Mshama ametoa agizo hilo wakati alipokutana na viongozi wa wafanyabiashara wa minadani , akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya , pamoja Timu ya dharula ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko RRT ambapo kabla ya kutoa agizo hilo elimu ya kujikinga na ugonjwa huo ilitolewa kwa wafanyabiashara hao.

Shukuru Kimaro na Dkt. Sabnus Ndunguri ni wajumbe kutoka Timu ya dharula ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko RRT ya halmashauri ya mji wa kibaha wakatoa elimu ya jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa COVD 19.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wameiomba serikali kuongea na taasisi za fedha ili ziweze kuangalia namna ya kuwasidia kupeleka marejesho ya mikopo kwani baadhi yao wamekopa katika taasisi hizo na hivyo kufunga kwa biashara zao kutaathiri marejesho ya mikopo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wagonjwa wa Kifua Kikuu waongezeka mkoani Tanga.

Read Next

Wahamiaji haramu 36 wakamatwa mkoani Mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!