Mwandishi Mkongwe wa habari za michezo Asha Muhaji afariki.

Aliyekuwa Afisa Habari wa klabu ya soka ya Simba Asha Muhaji amefariki dunia leo mchana wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za kifo cha zilizotolewa na familia yake, Marehemu Asha alilazwa hospitalini tangu alhamisi iliyopita hadi leo umauti ulipomfika.

Taarifa hizo pia zinaeleza kuwa, Mazishi yatafanyika kesho kwenye makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni Dar es Salaam, na msiba upo nyumbani kwa wazazi wake Mabatini Kijitonyama, huku mwili wa Marehemu Asha ukiwa umehifadhiwa katika msikiti wa Mahmuru Upanga ambapo ndipo itakapofanyika swala kabla ya mazishi.

Enzi za Uhai wake Marehemu Asha ambaye alikuwa mwandishi wa habari za michezo, aliwahi kufanya kazi kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Gazeti ya la Uhuru, pia akiwahi kuwa mhariri wa michezo katika gazeti la Rai.

Comments

comments

clement

Read Previous

BREAKING NEWS: Wagonjwa wapya watatu waongezeka Kenya.

Read Next

Madaktari 1,000 walioajiriwa kupangiwa mikoa yenye uhitaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!