Serikali yapokea msaada kukabiliana na Corona.

Serikali imepokea msaada wa vifaa-tiba kutoka China kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na maambukizi ya homa ya mapafu inayoambukizwa na kirusi kipya aina ya Corona (COVID-19).

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Muhammed Bakari Kambi amesema msaada huo ambao umetolewa na Taasisi ya Jack Ma na Alibaba ni pamoja na mavazi (PPE) 1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia watu waliobainika kuwa na homa hiyo, vitendanishi (Rapid Tests) 20,000 na Barakoa (Masks) 100,000.

Prof. Muhammed Kambi amesema msaada huo utawasaidia wataalamu wa afya nchini wakati wa kuwahudumia waliobainika na watakaobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Katika hatua nyingine, Prof. Muhammed Kambi amemshukuru Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia Ethiopia Tewodros Girma ambaye amekabidhi msaada huo kwa niaba ya Balozi wa nchi hiyo, Yonas Yosef.

Comments

comments

clement

Read Previous

Agizo la rais Magufuli latekelezwa kwa ubunifu Handeni.

Read Next

BREAKING NEWS: Wagonjwa wapya watatu waongezeka Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!