Wagonjwa wa Kifua Kikuu waongezeka mkoani Tanga.

Katika kufanikisha mikakati ya miaka mitano ya serikali ya kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu, Mkoa wa Tanga umefanikiwa kuwabaini wagonjwa wapatao 3,521 ikiwa ni ongezeko la wagonjwa 750 katika kipindi cha mwaka mmoja, na kuufanya mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya wagonjwa hao.

Mkoa wa Tanga ni kati ya mikoa yenye idadi kubwa ya wagonjwa wa kifua kikuu kutokana na juhudi za kuwadodosa wagonjwa hao kuanzia ngazi ya Jamii kwa kuwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma ngazi ya Jamii.

Dkt. Raphael Mumba ni Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Mkoa wa Tanga yeye anaelezea hali ilivyo kwa sasa katika Mkoa huu.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga wameelezea elewa wao juu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Aidha kwa upande mwingine Dkt, MUMBA amebainisha muingiliano wa ugonjwa wa Kifua kikuu pamoja na Corona kwa kuitahadharisha Jamii juu ya kuwalinda makundi maalum yaliyo kwenye hatari ya kuathirika na ugonjwa huo.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “WAKATI NI HUU TUUNGANISHE NGUVU NA KUWAJIBIKA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU”.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mvua zasitisha mawasiliano Ruvuma.

Read Next

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha asimamisha mnada mwezi mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!