Wazee wa Kimila kufanya maombi dhidi ya Corona.

Wazee wa Kimila na maarufu katika kata ya Mwada kijiji cha Sangaiwe Wilayani Babati wamesemakuwa wamejipanga kufanya maombi ya kimila ikiwa ni hatua ya wazee hao kuungana na watanzania wengine kuliombea taifa kuepukana na madhara makubwa ya mlipuko wa ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na Virusi Vya Corona.

Wazee kijijini hapa wamesemakuwa maombi hayo ya kimila imekuwa ni desturi na yenye kuleta matokeo chanya yanapofanyika pindi itokeapo mlipuko wa magonjwa pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Jamii zzishio kijijini hapa nao wameeleza kutambua maombi hayo ya kimila wakiwemo Vijana huku pia wakieleza kuwa mlipuko wa virus vya Corona kumeathiri shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ukosefu wa mahitaji muhimu ya nyumbani mara baada ya uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Babtai kusitisha shughuli minada yote kuendelea.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Babati Khamis Malinga amekiri kusitishwa kwa minada hiyo lakini akaeleza kuwa wapo mbinoni kuruhusu tena shughuli hizo kuendelea mara baada ya taharuki kubwa kwa wananchi kupungua.

Comments

comments

clement

Read Previous

Aliyevuka kwa kutoa Rushwa akamatwa.

Read Next

Agizo la rais Magufuli latekelezwa kwa ubunifu Handeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!